Main Article Content

Mwaka Kogwa Na Changamoto Zake


M Mohamed

Abstract

Kila jamii ina jadi yake ambayo inaweza kutumika katika kuitofautisha jamii hiyo na jamii zingine, za karibu au za mbali. Makunduchi ni miongoni mwa maeneo yanamozungumzwa lahaja za Kiswahili. Lahaja inayozungumzwa katika eneo hili inaitwa Kimakunduchi. Miongoni mwa matukio muhimu ya kijadi yanayofanyika katika jamii ya Makunduchi ni sherehe za Mwaka Kogwa. Kwa Wamakunduchi hizi ni sherehe kubwa kuliko sherehe nyingine yoyote inayofanyika katika jamii hii. Wamakunduchi kutoka sehemu mbalimbali hukusanyika katika uwanja wa Mwaka Kogwa ili kutekeleza jadi yao. Sherehe hizi pia huhudhuriwa na watu mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia.

             Makala haya yanakusudia kufafanua dhana ya Mwaka Kogwa kwa ujumla, dhima zake, changamoto zinazoikabili na kisha kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto hizo. Makala yamegawanywa katika sehemu tano. Sehemu ya kwanza  inajadili usuli wa  Mwaka Kogwa. Sehemu ya pili  inafafanua  dhima ya Mwaka Kogwa. Sehemu ya tatu inafafanua changamoto mbalimbali zinazozikabili sherehe za Mwaka Kogwa kwa sasa. Sehemu ya nne  ni mapendekezo ya nini kifanyike ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza. Sehemu ya tano na ya mwisho ni hitimisho.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886