Main Article Content

Maadili Ya Utafiti


M Mukuthuria

Abstract

Maadili ni kaida zinazoelekeza tabia zetu katika mahusiano yetu ya kila siku na wenzetu (taz. Mathooko na wenzie, 2007:15).  Katika utafiti, maadili ni uwajibikaji na uwelekevu kitabia kuhusiana na haki za wale wote tunaotangamana nao katika utafiti, uwelekevu katika nia na malengo ya utafiti na jinsi ya kutumia matokeo kwa uadilifu ili yaweze kuwa na faida kwa jamii ya binadamu.  Suala hili ni la msingi na ndilo limepewa kipaumbele katika makala haya.  Katika kulishughulikia, tutafafanua ni kwa sababu gani  maadili yazingatiwe, wanaotakiwa kuzingatia maadili wakati wa utafiti, tutaangalia ni lini tuanze kuzingatia maadili, masuala ya kimaadili yanayoweza kuibuka na athari za utovu wa maadili katika utafiti; hatimaye, mikondo ya kimkabala au ya kinadharia kuhusiana na utekelezaji wa maadili nyanjani itazingatiwa.  Inakisiwa kwamba kufikia mwisho wa sura hii, umuhimu wa suala la maadili katika utafiti wowote ule litabainika na hasa ufahamu wa ni kwa nini utafiti wa lugha utilie maanani suala hili kama taaluma zingine za kisayansi.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886