Main Article Content

Majigambo Ya Wanawake: Je, Yapo?


M Samwel

Abstract

Kwa muda mrefu, utanzu wa majigambo umekuwa ukichukuliwa kuwa ni utanzu wa wanaume. Utanzu huu, umehusishwa na ushujaa, ujasiri na ushupavu ambao inaaminika wanawake hawana na hawawezi kuwa nao. Wanawake, kwa upande wao, wamekuwa wakidaiwa kuwa hawana majigambo bali wao huimba tondozi. Makala haya, yanatoa ripoti ya utafiti uliofanyika katika mkoa wa Kagera miongoni mwa kabila la Wahaya. Matokeo ya utafiti huo yanatushawishi kujiuliza upya; je, majigambo ya wanawake yapo au hayapo? Swali hili linatokana na ukweli kwamba, data za uwandani zinatushawishi kuamini kwamba majigambo ya wanawake yapo.

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886