Main Article Content

Nafasi Ya Lugha Za Asili Katika Shirikisho La Afrika Mashariki


YP Msanjila

Abstract

Makala haya yanajadili nafasi ya lugha za asili katika Shirikisho la Afrika Mashariki. Lugha ni sehemu muhimu ya utamaduni wa jamii yoyote ile. Kijamii, lugha za asili zina nafasi ya kutumiwa katika Shirikisho kutokana na sababu zifuatazo: Kwanza, ukiachilia mbali lugha za taifa za asili, lugha nyingi za asili katika Shirikisho zinatumiwa sana na wakazi wa vijijini. Inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 70 ya wazungumzaji wa lugha za asili wanaishi vijijini. Pili, lugha za asili zina dhima ya kukuza istilahi za fani mbalimbali. Tatu, lugha za asili ni msingi imara wa kujenga utamaduni wa Mwafrika, na nne, lugha za asili zinadumisha utambulisho wa Mwafrika katika Shirikisho. Kutokana na sababu hizi, kuna haja ya kuzitambua rasmi lugha za asili katika sera ya lugha ya Afrika Mashariki kama lugha muhimu za mawasiliano katika Shirikisho.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886