Main Article Content

Mabadiliko ya Kiuimbaji ya Nyimbo za Ibada katika Kanisa Katoliki Tanzania: Uchunguzi wa Makanisa Teule


Kassomo Athanas Mkallyah

Abstract

Makala haya yanahusu mabadiliko ya kiuimbaji ya nyimbo za  bada na athari zake katika Kanisa Katoliki, Tanzania. Makanisa  mawili ya kikatoliki ya Dar es Salaam yalichunguzwa, Kanisa  Kuu la Mtakatifu Yosefu na Kanisa la Mtakatifu Paulo Mtume  Ubungo-Msewe. Makanisa haya yalichaguliwa kutokana na kuwepo kwa wamisionari wageni na wazawa waliosaidia  kupatikana kwa taarifa muhimu za utafiti uliofanyika. Njia  zilizotumika kukusanya data ni utalii wa uwandani, mahojiano  na majadiliano. Utafiti uliofanyika ulilenga kujibu maswali yafuatayo: ni mabadiliko gani ya kiuimbaji yaliyotokea katika  nyimbo za ibada za kikatoliki Dar es Salaam? Ni mambo gani  yaliyosababisha mabadiliko ya uimbaji wa nyimbo za ibada  katika Kanisa Katoliki Dar es Salaam? Data zilizokusanywa zilichambuliwa kwa kutumia Nadharia ya Utendaji. Matokeo ya  utafiti yalionesha kuwa yapo mabadiliko katika muktadha  wa utunzi wa nyimbo, maudhui, lugha, na waimbaji wa nyimbo  yaliyoleta uhuru wa kusali kwa Watanzania na  kulijenga kanisa lao. Mabadiliko haya yalisababishwa na  kupatikana kwa uhuru wa Tanzania Bara, Mtaguso wa  Vatikano II, utamadunisho, biashara na kukua kwa sayansi na  teknolojia Tanzania. 


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129