Main Article Content

Utendaji wa Wahusika Wakuu wa Fasihi ya Watoto ya Kiswahili: Uchunguzi wa Riwaya ya <i>Ngoma ya Mianzi</i>


Saumu Mkomwa

Abstract

Makala haya yanayohusu utendaji wa wahusika wakuu wa  fasihi ya watoto ya Kiswahili ni sehemu ya utafiti uliofanywa  kwa ajili ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu  cha Dodoma. Data za utafiti zilipatikana uwandani na maktabani kwa kusoma riwaya teule na kufanya usaili na  mwandishi wa riwaya hiyo na wataalamu wa fasihi ya watoto.  Data hizo zilichanganuliwa kwa mbinu ya kimaudhui kwa  sababu utafiti ulikuwa wa kitaamuli. Nadharia ya Saikochanganuzi ya Sigmund Freud (1856-1939) ilitumika  katika uchanganuzi huo. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa  utendaji wa wahusika wakuu unaweza kudhihirika kwa mtindo  wa kuhoji, kutaarifu, kushauri, kudadisi na kuonya. Mtindo huu umebainika kutokana na mazungumzo baina ya  wahusika na masimulizi ya kiutendaji yanayokwenda  sambamba na mazungumzo hayo. Kwa mujibu wa Mbunda  (1993), lugha ya mazungumzo huwekwa katika riwaya ili isimchoshe msomaji, ambaye katika muktadha wa makala  haya, ni mtoto wa miaka 15 hadi 18. Mtafiti anapendekeza  watunzi, wahakiki na wataalamu wa kazi za fasihi, hususani  fasihi ya watoto kutafiti mitindo hii katika riwaya nyingine za  watoto.


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129