Main Article Content

Mhusika Sauti katika Tamthilia ya Kimya Kimya Kimya ya Said A. Mohamed


Collins Kenga Mumbo
Anne Mwari

Abstract

Makala haya yanalenga kudadisi sauti na uhusika wake  kwenye uwasilishaji wa ujumbe katika tamthilia ya Kimya  Kimya Kimya ya Said A. Mohamed (2011). Sauti kama  mojawapo ya vipengele vya utendaji imetumiwa katika kazi tofautitofauti za tamthilia kwa sababu mbalimbali kutegemea  mahitaji ya mtunzi wa kazi ya sanaa. Sauti inaweza kutekeleza  jukumu kubwa inaposhirikishwa vilivyo katika tamthilia. Hata  hivyo, watunzi wengi wanatumia sauti kwa ajili ya kushereheshea jambo fulani, kusisitizia ujumbe na kutoa  maoni kuhusu wazo kuu linalolengwa hadhira. Wakati  mwingine sauti huwa inatumika kama kicheko au kuweka  utangulizi na kuhitimishia tamthilia. Kwa kuzingatia matumizi  hayo, ni bayana kuwa matumizi ya sauti katika tamthilia nyingi  bado hayajapewa uzito unaostahili. Kutokana na hali  hiyo makala haya yanachunguza namna sauti ilivyotumika  kama mhusika na uwasilishaji ujumbe kwa kurejelea tamthilia  ya Kimya Kimya Kimya. Hivyo, mbinu iliyotumika kukusanya  data za utafiti huu ni usomaji wa kina wa tamthiliya tajwa. Hii  ni tamthilia ya kipekee katika matumizi ya sauti, ambapo  mwandishi Said A. Mohamed amewajenga baadhi ya wahusika wake kama wahusika sauti. Amezifanya sauti sio tu kuongea  bali pia kushiriki kikamilifu katika majibizano na uigizaji na  wahusika wengine. Tumezingatia jinsi sauti ilivyotumika  kujenga na kukuza wahusika na uhusika katika tamthilia ya   Kimya Kimya Kimya kwa kujikita katika ushiriki wa mhusika   binafsi, uhusika wa makundi na njia zinazotumiwa na   wahusika sauti kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa na   mwandishi. Hatimaye, tumetathmini mchango wa sauti hizi  katika kufanikisha utendaji na uwasilishaji maudhui kwa  hadhira lengwa. 


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129