Main Article Content

Tathmini ya Nyimbo za Muziki wa Kizazi Kipya Karne ya 21 Nchini Tanzania: Tija na Madhara yake


Gervas A. Kasiga

Abstract

Makala haya yamefanya tathmini ya nyimbo za muziki wa  kizazi kipya wa karne ya 21 nchini Tanzania. Makala  yamechunguza tija na madhara ya muziki huu kwa wasanii na  hadhira. Vigezo vya kibiashara na kidhamira viliteuliwa  kushughulikia jambo hili. Kupitia tathmini, makala yamebaini  kuwa katika karne ya 21 muziki wa kizazi kipya umeweza  kufanikiwa kujenga mahusiano ya kifani na wasanii wa nje ya  Tanzania. Pia, imebaini kuwa muziki huu unasisitiza uwepo wa  mapenzi ya kweli katika jamii, unafariji, na kutia moyo kwa  waliokata tamaa. Tija nyingine za muziki wa kizazi kipya  zilizobainishwa ni uongezaji wa fursa za kiajira, utoaji wa  elimu, na uburudishaji. Isitoshe, makala yamebaini madhara  ya muziki huu yanayotokana na utumiaji wa lugha ya ufyosi,  uhamasishaji wa vitendo vya ngono, na uhamasishaji wa  kutumiwa mavazi yasiyofaa kwa hadhira. Vilevile, kufifisha  nafasi ya nyimbo zenye kufuata maadili ya Kitanzania  kusikilizwa na hadhira nalo limebainika kuwa ni suala  linaloletwa na madhara ya muziki huu. Mwisho,  imependekezwa kuwa ni vema kwa nyimbo za muziki wa kizazi  kipya wa karne ya 21 kuweka msisitizo zaidi katika  masuala yanayoweza kujenga jamii mpya ya Kitanzania kwa  namna bora.  


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129