Main Article Content

Uchanganuzi wa Tungo zenye Upinduzi wa Kimahali katika Lugha ya Kiswahili: Sifa za Muundo wa Taarifa na Sababu za Upinduzi wa Kimahali katika Mawasiliano


Fabiola Hassan

Abstract

Kuna uhusiano baina ya udarajia wa dhima za kisemantiki na dhima za kisarufi. Uhusiano uliopo ni kwamba kiambajengo  kilichopo katika nafasi ya juu katika udarajia huo ndicho  kinapaswa kuwa kiima na sio kiambajengo kilichopo katika nafsi ya chini. Tungo zenye upinduzi wa kimahali zinakiuka  uhusiano huo. Katika tungo hizo, kimahali, ambacho kipo  katika nafasi ya chini, kinakuwa kiima ilihali sio mtenda au  kithimu. Wataalamu mbalimbali wamefafanua tungo hizi  katika lugha za Kibantu. Licha ya kufanya hivyo, hakuna uwazi  kuhusu sifa za muundo wa taarifa na sababu za upinduzi wa  kimahali katika mawasiliano. Hivyo, makala haya yanafafanua  na kubainisha masuala hayo katika lugha ya Kiswahili. Data  zilizotumika zimepatikana kwa mbinu ya uchambuzi wa matini, upimaji wa usahihi wa kisarufi pamoja na usaili. Data hizo  zimefasiriwa kwa kutumia misingi ya Nadharia ya Sarufi Leksia  Amilifu (Bresnan na Kaplan, 1982). Baada ya kufasiri  data hizo, makala haya yanabainisha kwamba muundo wa  taarifa wa tungo hizi una aina mbili za taarifa, yaani mada na  fokasi. Aidha, makala yanafafanua kwamba upinduzi wa  kimahali unatokea kwa sababu ya umadaishaji wa kimahali na  ufokalishaji wa kithimu/mtenda. 


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129