Main Article Content

Changamoto za Kipragamatiki kwa Wanafunzi wa Kiswahili Nchini Rwanda


Mukamana Helene
Ntawiyanga Sylvain

Abstract

Makala haya yanalenga kuchunguza changamoto za  kipragmatiki kwa wanafunzi wa Kiswahili nchini Rwanda.  Ingawa wanafunzi Wanyarwanda wanajifunza lugha hii  kuanzia mwaka wa kwanza wa shule za sekondari,  imedhihirika kuwa wanapambana na changamoto mbalimbali  katika matumizi yao ya Kiswahili (Ntawiyanga, 2015). O'Keeffe  (2011) anafafanua kuwa ustadi wa kipragmatiki ni miongoni  mwa changamoto kubwa zinazowakabili wanaojifunza lugha  na kuwa ni vigumu kuukuza uwezo huu kwa sababu  maendeleo yake hayatokani na umilisi wa kisarufi. Makala  haya yameweka bayana changamoto za kipragmatiki kwa wanafunzi wa Kiswahili nchini Rwanda, sababu au vyanzo vya  changamoto hizo, na yametoa mapendekezo ya namna ya  kukabiliana nazo. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya  Urekebishaji Mawasiliano ya Giles (1973) ambayo inaweka  pamoja vipengele vya kisaikolojia na vya kijamii katika kuamua  mtindo wa mawasiliano yenye mwingiliano au  mtagusano wa kijamii. Mbinu zilizotumika kukusanya data za  utafiti huu ni hojaji pamoja na mahojiano. Wanafunzi wa  Kiswahili katika Ndaki ya Elimu, Chuo Kikuu cha Rwanda pamoja na wahadhiri wao ndio walioshirikishwa katika utafiti  huu. Kulingana na uchunguzi wa data iliyotumika katika  makala haya, imedhihirika kuwa wanafunzi wa Kinyarwanda  hukabiliwa na changamoto ambazo hutokana na uhamisho wa mitindo ya lugha kutoka Kinyarwanda hadi Kiswahili. Aidha,  imedhihirika kuwa vyanzo vingi vya changamoto hizi ni  kujifunzia Kiswahili nje ya utamaduni wake, kutojali mtindo  sahihi unaopaswa kutumiwa pamoja na ukosaji wa kielelezo  cha kufuatilia. 


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129