Main Article Content

Tathmini ya Anthropomofiki katika Riwaya ya Shamba la Wanyama


Waithiru Kago Antony
Sheila Wandera-Simwa
Onyango Ogola James

Abstract

Makala haya yanatathmini namna anthropomofiki ilivyotumika katika riwaya ya Shamba la Wanyama ya George Orwell. Orwell ni  miongoni mwa waandishi maarufu na waliosifika katika fani na utunzi wa kazi za fasihi zinazokashifu mfumo wa utawala wa kibepari, kwa  kutumia mbinu ya anthropomofiki. Lengo kuu la makala haya ni kujadili jinsi ambavyo anthropomofiki imetumiwa na mwandishi  katika kukabiliana na ubepari ulimwenguni. Hivyo, makala haya yanajikita katika kujadili mapinduzi yaliyozalishwa na elimu na  yaliyowasilishwa kianthropomofiki na George Orwell. Katika kufanikisha tathmini hii, makala haya yaliongozwa na baadhi ya mihimili  mikuu ya nadharia ya Uhakikimazingira kama ilivyoasisiwa na Glotfelty, Fromm pamoja na Buell. Mihimili miwili mikuu iliyoongoza tathmini ya makala haya ni uwezo na kifo, na uongozi mbaya na ukoloni mamboleo. Nadharia hii imejikita katika uhakiki wa matini za  kifasihi kwa kudhihirisha uhusiano na utegemeano baina ya binadamu na mazingira. Data ya makala haya ilipatikana maktabani.  Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa mwandishi amefanikiwa kukemea ubepari kupitia mbinu ya anthropomofiki katika riwaya teule.  Riwaya hii iliteuliwa kwa kudhamiria kutokana na kuwepo kwa suala la mazingira ya binadamu kupitia mbinu ya anthropomofiki. 


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129