Main Article Content

Changamoto Zinazowakabili Walimu katika Ufundishaji wa Kiswahili katika Shule za Upili Nchini Kenya


Lina Akaka

Abstract

Maendeleo ya lugha au somo la Kiswahili katika nyanja za elimu nchini Kenya, kabla na baada ya uhuru, yalitegemea mapendekezo ya tume zilizoundwa. Baadhi ya tume hizo zilikitambua Kiswahili ingawa kwa kukipa nafasi ya pili baada ya lugha ya Kiingereza. Jambo hili lilitokea kwa sababu Kiingereza kilikuwa kimeshapewa hadhi ya kuwa lugha rasmi kwa hivyo kikawa lugha ya kufundishia katika viwango vyote vya shule na vyuo isipokuwa kwa darasa la kwanza hadi la tatu (Chimerah, 1998). Wakoloni waliotawala Kenya, tofauti na walioitawala Tanzania, hawakukistawisha Kiswahili. Tume za elimu zilizoundwa kutathmini masuala ya elimu wakati wa enzi za ukoloni zilikipuuza Kiswahili katika sera za elimu na kuzipa hadhi lugha za kimakabila pamoja na Kiingereza. Changamoto wanazokumbana nazo walimu wa Kiswahili wanapofundisha Kiswahili katika shule za upili zitajadiliwa kwa misingi ya sera ya elimu na motisha kutoka kwa wadau kama vile wachapishaji, walimu wakuu, wanafunzi wenyewe na vyuo vikuu ambavyo huandaa walimu kufundisha katika kiwango hicho. Matatizo yatakayoshughulikiwa ni pamoja na mbinu zinazotumiwa katika ufundishaji wa Kiswahili, vifaa vya kufundishia na changamoto zinazotokana na sera ya elimu kuhusu somo hili pamoja na suala la uchapishaji.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X