Author Guidelines

KIOO CHA LUGHA ni jarida la Kimataifa la Taasisi ya Taaluma za Kiswahili linalochapisha makala za lugha, fasihi na isimu. Jarida huchapishwa katika Juzuu moja kila mwaka. Makala inaweza kuandikwa katika lugha ya Kiswahili au Kiingereza.

 

Makala: Waandishi wanaombwa kuwasilisha nakala ngumu mbili za kila makala na nakala-tepe kwa kutumia anwani ya barua-pepe ya iks@udsm.ac.tz au ya wahariri husika. Makala inapaswa kuwa na kichwa cha makala, jina la mwandishi, Chuo au Taasisi anayofanyia kazi, anwani ya posta, namba ya simu pamoja na barua-pepe. Taarifa hizi ziandikwe juu kwenye ukurasa wa kwanza.  Makala iwe imechapwa kwa kutumia programu ya Word, kukiwa na nafasi 1.5 kati ya mstari na mstari, na kukiwa na pambizo pana pande zote. Ikisiri isiyozidi maneno 150 iwe mwanzoni mwa makala chini ya taarifa zilizotajwa hapo juu.

 

Makala itatathminiwa na walau wasomaji wawili bila kuonesha mwandishi ni nani. Epuka utambulisho wowote kumhusu mwandishi, ili wanaoitathmini wasimfahamu mwandishi. Kwa watakaotuma kwa njia ya posta makala itarejeshwa kwa mwandishi pale tu ambapo gharama za usafirishaji zimelipwa. Waandishi ambao makala yao itakubaliwa kuchapishwa, watapatiwa nakala moja ya Jarida lenye makala yao pamoja na malopoo kumi ya makala.

Mifano katika makala: Mifano yote, iwe ya isimu au fasihi, inapaswa kuandikwa kwa herufi koza au kwa italiki, na haina budi kufuatwa na `maana’ yake kama inahitajika. Kwa wanaisimu, ishara zinazoruhusiwa ni zile za Alfabeti ya Kifonetiki ya Kimataifa. Iwapo kutakuwa na haja ya kuwa na ishara tofauti ziandikwe kwenye ukurasa tofauti.

 

Tanibichini au Tanibimwisho: Tanbihi zitumiwe kwa uwekevu; zisiwe nyingi. Kama mwandishi anatumia tanbihi za mwisho wa makala, zichapwe kwenye ukurasa husika, zikiwa zimeorodheshwa kwa namba.

 

Marejeleo: Utaratibu wa marejeleo uliozoeleka kwa majarida mbalimbali ndio utumike. Kurejelea andiko katika matini kufanyike kwa kuanza na mwandishi, kisha mwaka na mwisho ukurasa, k.m. Mulokozi (1996:34) au (Mulokozi, 1996:35).

 

Mwishoni mwa makala, marejeleo yaliyotajwa katika andiko yapangwe kiabjadi. Majina ya vitabu na majarida yaandikwe kwa italiki na yale ya makala yawekwe kwenye ‘alama za kufungua na kufunga semi’ kama inavyooneshwa hapa:

 

Mulokozi M.M. (1996).  Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Mekacha, R.D.K. (1997). ‘Disconnecting Education,’  katika Journal of Linguistics and Language in Education, 3:95-105. Dar es Salaam: Idara ya Lugha ya Kiswahili na Isimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

 

Majedwali, michoro, ramani na picha vipangwe kwa unadhifu kwenye ukurasa. Mahali pa kuweka majedwali, michoro au ramani paoneshwe kwa uwazi. Majedwali au michoro isiyokaa vizuri kwenye ukurasa mmoja haitachapwa.

 

Makala za jarida hili zinapatikana pia Mkondoni kupitia tovuti ya www.udsm.ac.tz na pia katika mkondo wa  Majarida ya Kiafrika  www.ajol.info.


INSTRUCTIONS TO CONTRIBUTORS

 

KIOO CHA LUGHA is an international journal published by the Institute of Kiswahili Studies (IKS). The journal is devoted to the study of Kiswahili Language, Linguistics and Literature. It is published once a year. We accept scholarly papers and articles written in Kiswahili or English.

 

Submissions should be made in soft or hard copy, by either sending two hard copies to IKS mailing address or sending soft copy to iks@udsm.ac.tz or respective journal editors. The first page of the paper manuscript should include the title of the paper, author’s name, institution, postal address, phone number and email. A paper should be typed, 1.5 spaced on A4 size paper and normal margins on all sides. Also, the paper should bear an abstract of not more than 150 words just after the author’s information.

 

All our articles go through a double-blind review process. Authors must avoid putting their personal identification in the article so as to avoid reviewers’ bias. Papers which were submitted via mailing address will be sent back to the authors after they have paid postage cost. The author whose paper will be accepted for publication will receive a free copy of the journal and ten offprints of his/her paper.

 

Examples in the paper: All examples used in a paper have to be bold faced or italicized, and have to be elaborated if necessary. The linguists are allowed to use the International Phonetic Alphabets. If there is a need to have any other symbols, they have to be written in a separate page. 

 

Footnote and Endnote: Footnotes and endnotes have to be used to a minimum. Endnotes should appear just before the bibliography and have to be arranged in a numerical order.

 

Citation and Reference format guidelines: When mentioning references in the text, cite only the last name of the author followed by the date of publication and page(s), e.g. Mulokozi (1996:34) or (Mulokozi, 1996:35).

 

All references mentioned in the text have to appear at the end of the paper and should be in alphabetical order. Names of the books and journals have to be in italic, and names of the papers have to be in quotation marks as shown below:

 

Mulokozi, M.M. (1996).  Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Mekacha, R.D.K. (1997). ‘Disconnecting Education,’  katika Journal of Linguistics and Language in Education, 3:95-105. Dar es Salaam: Idara ya Lugha ya Kiswahili na Isimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

 

Tables, drawings, maps, illustrations, photos and pictures have to be neatly arranged in a respective page. A specified position to put the tables, drawings and maps have to be clearly shown. Tables and illustarations which are not well set on a page will not be published.

 

Papers for this journal are available on www.udsm.ac.tz and  www.ajol.info   

Privacy Statement

The names and email addresses entered in this journal site will be used exclusively for the stated purposes of this journal and will not be made available for any other purpose or to any other party.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X