Main Article Content

Asili na Chimbuko la Wazungumzaji wa Kimakunduchi: Hoja za Kihistoria


Mussa M. Hans

Abstract

Wakati tukiwa tunasherehekea mafanikio ya lugha ya Kiswahili katika nyanja mbalimbali, hatuna budi kujiuliza katika mijadala yetu ni kwa kiwango gani tumezishirikisha lahaja za Kiswahili katika kubaini mambo mbalimbali ikiwemo historia ya lugha hii. Tukumbuke kwamba wakati wa uteuzi wa lahaja ya Kiunguja kuwa msingi wa usanifishaji wa Kiswahili, ilishauriwa kwamba lahaja nyinginezo za Kiswahili zishirikishwe ipasavyo katika ukuzaji wa lugha ya Kiswahili. Hata hivyo, kwa muda mrefu sasa maendeleo ya lugha ya Kiswahili yamekuwa yakijadiliwa bila ya kuzishirikisha lahaja za lugha hii. Matokeo yake ni kwamba kuna hazina kubwa iliyomo katika lahaja hizi ambayo haijatumiwa ipasavyo katika mchakato wa kukuza lugha ya Kiswahili. Miongoni mwa maeneo yenye mjadala mkali na ambayo lahaja zikishirikishwa vema zinaweza kuwa na mchango mkubwa ni katika historia ya lugha ya Kiswahili, hususani mjadala kuhusu asili na chimbuko la lugha hii. Kwani wataalamu mbalimbali wamekuwa wakihitilafiana kuhusu mahali hasa wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili walipotokea. Lengo la makala haya basi ni kujadili kuhusu chimbuko la wazungumzaji wa lahaja ya Kimakunduchi visiwani Zanzibar.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X