Mitindo ya Lugha katika Tovuti za Serikali Nchini Tanzania na Athari zake katika Usambazaji wa Taarifa kwa Umma

  • Rhoda P. Kidami

Abstract

Tovuti ni miongoni mwa vyanzo vinavyotumiwa na serikali ya Tanzania kusambaza taarifa kwa jamii. Lugha rasmi, yaani Kiswahili na Kiingereza, ndizo zinazotumiwa kwa usambazaji huo. Baadhi ya tovuti zina sehemu ya kuchagua lugha, hivyo, mtumiaji ana uhuru wa kuchagua lugha mojawapo kati ya hizo mbili. Katika makala hii tumechunguza jinsi lugha hizo zinavyotumiwa kwa pamoja kusambaza taarifa kwa umma wa Tanzania na duniani kote kwa ujumla. Kurasa za Kiswahili na za Kiingereza zilizomo ndani ya tovuti moja zimechunguzwa na kubainisha mitindo ya lugha inayotumiwa kisha kutathmini athari za mitindo hiyo katika usambazaji wa taarifa kwa umma. Uchunguzi huo umeongozwa na Mkabala wa Reh (2004) unaohusu aina za maandishi ya kijamiilughaulumbi katika jamii zenye wingilugha. Data zilikusanywa kutoka katika tovuti za wizara za serikali ya Tanzania. Tovuti zilizohusishwa ni zile zenye sehemu ya uchaguzi wa lugha ili kuwezesha ulinganishi wa matumizi ya lugha kati ya kurasa za Kiswahili na zile za Kiingereza. Matokeo ya utafiti huu yanadhihirisha matumizi ya lugha mseto kati ya Kiswahili na Kiingereza yaliyopo katika mtindo wa ujalizaji. Mtindo huu ni faafu kwa watumiaji wenye uelewa wa lugha zote mbili ilhali kwa wenye uelewa wa lugha moja, yaani Kiswahili au Kiingereza, watapata baadhi tu ya taarifa.
Published
2020-02-14
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X