Main Article Content

Kilongo cha Unyanyasaji wa Kiusemi katika Mahusiano ya Vijana katika Tamthilia ya <i>Hatia</i>: Mkabala wa Uchanganuzi Tunduizi Kilongo wa Kifeministi


Boaz Mutungi

Abstract

Makala hii imetumia tamthilia ya Hatia katika kufafanua kilongo cha unyanyasaji wa kiusemi baina ya vijana wanaokuwa katika mahusiano ya kutongozana. Unyanyasaji huu unawaathiri vijana wengi. Suala hili linafaa kuchunguzwa kwa sababu vijana wanyanyasaji wanasemekana kuendeleza tabia hiyo hata baadaye katika ndoa zao. Ukilinganishwa na aina nyingine za unyanyasaji katika mahusiano, unyanyasaji wa kiusemi unajitokeza zaidi katika jamii, na madhara yake ni hatari zaidi. Aidha, fasihi inaiga mambo yanayotokea katika jamii huku ikilenga kuboresha jamii hiyo. Vilevile, lugha ya tamthilia inalingana na ya mazungumzo ya kawaida kwa sababu zote zinarejelea mitagusano ya kijamii ambapo wahusika hujibizana moja kwa moja. Kwa kutumia Nadharia ya Uchanganuzi Tunduizi Kilongo wa Kifeministi, makala inadhihirisha kwamba mbali na mamlaka au nguvu za kijinsia, kilongo cha unyanyasaji wa kiusemi kinajikita katika madaraka ya kiumri na ushupavu maalumu wa mhusika au kundi mahususi. Misingi hiyo ya kimamlaka imemwezesha kijana wa kiume kumpuuza, kumkanganya, na hivyo kumdhibiti kwa urahisi kijana wa kike.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X