Ushujaa katika Motifu ya Safari ya Msako na Utamaduni na Falsafa ya Kiafrika

  • Felix K. Sosoo

Abstract

Utamaduni ni mfumo wa maisha au jinsi watu wanavyoishi katika jamii fulani. Mfumo huu unaundwa na vipengele mbalimbali kama  vile mavazi, lugha, sanaa za maonyesho, imani, mila desturi, na kadhalika. Lengo la makala hii ni kuchunguza namna ushujaa katika motifu ya safari ya msako unavyoakisi utamaduni na falsafa ya Kiafrika ukilinganishwa na mtazamo na maoni ya wataalamu na watafiti mbalimbali kuhusu falsafa ya Kiafrika. Swali linaloulizwa na wengi ni: je, ni kweli kuna falsafa ya Kiafrika? Kwa vile lengo katika makala hii ni kuchambua utamaduni na falsafa ya Kiafrika vinazojitokeza katika ngano za Kiewe na riwaya teule za Shaaban Robert, ni vizuri kwanza kuthibitisha kama kuna falsafa ya Kiafrika katika riwaya teule na ngano za Kiewe. Vipengele vya ontolojia vilivyoshughulikiwa katika makala hii ni: uzazi, umoja na mshikamano, uchawi na uganga (sihiri), na imani katika kifo na roho (maisha baada ya kifo). Vipengele hivi vya falsafa ya Kiafrika vimechambuliwa kuonesha namna vinavyosawiriwa katika ngano teule za Kiewe na riwaya moja ya Shaaban Robert ambayo ni Kufikirika.

Published
2021-05-04
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X