Main Article Content

Mchango wa Mathias Mnyampala katika maendeleo ya ushairi wa Kiswahili


Anna N. Kyamba

Abstract

Makala hii inakusudia kuchunguza mchango wa Mathias Mnyampala katika maendeleo ya ushairi wa Kiswahili. Mnyampala ni miongoni mwa washairi maarufu wa ushairi wa Kiswahili katika karne ya ishirini. Kwa ujumla, mchango wa Mnyampala katika ushairi wa Kiswahili haujulikani kikamilifu tukilinganisha na washairi wengine kama Muyaka bin Haji na Shaaban Robert. Maswali tunayojiuliza ni kwamba: kwa nini Mnyampala hajazungumziwa na wataalamu mbalimbali? Mnyampala alikuwa na mchango gani katika ushairi wa Kiswahili? Kutokana na maswali hayo tunaona kuna haja ya kuchunguza mchango wa mtaalamu huyu katika ushairi wa Kiswahili. Hivyo, katika makala hii tunabainisha mchango wa Mnyampala (akiwa mshairi wa mwanzo wa miaka ya 1960 anayetoka sehemu za bara) katika maendeleo ya ushairi wa Kiswahili kimaudhui na kifani. Data zilizomo ndani ya makala hii zimetokana na mbinu ya maktabani na mahojiano na watafitiwa nyanjani kuhusu maisha, historia ya Mnyampala, kazi zake zilizochapishwa na miswada yake isiyochapishwa ambayo ni: Hazina ya Washairi, Mahadhi ya Kiswahili na Mashairi ya Vidato.


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X