Main Article Content

Uainishaji wa Ngeli za Nomino za Kivunjo Kimofolojia


Ruth N. Shao
Salome J. Kotira

Abstract

Makala hii inashughulikia uainishaji wa ngeli za nomino katika lugha ya Kivunjo na kubainisha idadi yake kimofolojia. Ili kutimiza malengo haya, mbinu ya usampulishaji nasibu pangilifu imetumika katika kuwateua watoataarifa ambao ni wazungumzaji wa Kivunjo. Data zimekusanywa kwa kutumia hojaji, usaili na ushuhudiaji. Mkabala mseto, yaani wa kimaelezo na kiidadi umetumika katika kuwasilisha na  kuchanganua data za utafiti huu. Aidha, utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Mofolojia Asilia (NMA) iliyopendekezwa na Dressler (1985) na Wurzel (1987). Pamoja na nadharia hii, mkabala wa Viambishi Awali vya Nomino umetumika kubainisha viambishi ngeli vya  nomino katika misingi ya umoja na wingi. Hivyo, kwa kutumia Mkabala wa Viambishi Awali vya Nomino matokeo ya utafiti huu   yamebainisha kuwa lugha ya Kivunjo ina ngeli 18.


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X