Fasihi ya Kiswahili ya Majaribio: Makutano ya Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi

  • F.E.M.K Senkoro University of Dar es Salaam

Abstract

Makala hii inatalii maana ya fasihi ya Kiswahili ya majaribio, kwa kupitia kanuni za kifasihi simulizi ambazo zinaelekea kuwa msingi na mwimo wa majaribio hayo. Makala inaonyesha kuwa kanuni hizi ndizo ambazo zimejidhihirisha hata katika fasihi ya Kiswahili ya hivi karibuni ya waandishi waliofanya majaribio ya aina mbalimbali, wakiwemo wa tamthilia, riwaya na hadithi fupi. Makala inatumia zaidi mifano kutoka katika tamthilia za Lina Ubani (P. Muhando) na Jogoo Kijijini na Ngao ya Jadi (E. Hussein) na pia riwaya ya Rosa Mistika (E.Kezilahabi) kueleleza majaribio hayo. Swali ambalo hatimaye linajadiliwa ni, je, majaribio haya yanafuata kanuni zipi? Upya una nafasi gani katika majaribio? Na, je, majaribio mahsusi ya fasihi fulani yanaanza na kuisha wakati gani?

Author Biography

F.E.M.K Senkoro, University of Dar es Salaam
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Kiswahili
Published
2010-10-23
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X