Main Article Content

BAADHI YA VIPINGAMIZI VYA KIUTAWALA VYA KUTUMIA KISWAHILI KUFUNDISHA SEKONDARI NA VYUO


M.M Mulokozi

Abstract

Makala hii inaeleza kwa undani jinsi vipingamizi vya kiutawala vinavyokwamisha juhudi za kutumia lugha ya Kiswahili katika kufundishia shule za sekondari na vyuo. Vipingamizi hivyo ni pamoja na migogoro ya sera, ukosefu wa msukumo wa kisiasa na kisheria, kasumba, udhaifu wa vyombo vya kukuza Kiswahili na shinikizo kutoka nje. Pia, makala inatoa mapendekelezo kadhaa ili Kiswahili kiweze kutumika kama lugha ya kufundishia katika sekondari na vyuo. Baadhi ya mapendekezo hayo ni; utekelezaji wa programu ya mwaka 1999, kuanzisha shule chache za sekondari za majaribio zitakazotumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia na kuunda sheria zitakazohimiza matumizi ya Kiswahili. Aidha, marekebisho ya katiba yazingatie umuhimu wa Kiswahili kama lugha ya Taifa na matatizo ya asasi mbalimbali zinazohusika na ukuzaji wa lugha ya Kiswahili yashughulikiwe kitaifa hususani kwa kuongeza bajeti katika asasi hizo.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X