ULINGANISHI WA MUUNDO WA VITOMEO KATIKA KAMUSI MBILI ZA KISWAHILI - KIINGEREZA

  • E.K.F Chiduo University of Dar es Salaam

Abstract

Ulinganishi wa Kamusi Sanifu ya Kiswahili-Kiingereza (KSKK, 1993) na Kamusi ya Kiswahili- Kiingereza (KKK, TUKI 2001) unazingatia mtazamo wa Nkweti-Azel. Mtizamo huu unazingatia vipengelele vikuu vinane vilivyogawanyika katika vipengele vidogo 21: (i) Otografia ( Kitomeo, kibadala, kisawe) (ii) Fonolojia (matamshi) (iii) Mofolojia na Sintaksia ( viambiasi wingi, ngeli za nomino, vinyambuo, uelekezi) (iv) Kategoria za maneno (v) Pragmantiki (tahadharia ya matumizi alama za rejesta za kijiografia) (vi) Etimolojia (asili, maneno husiani) (vii) Fasiri ( fasiri ya maneno, mifano muktadha) (viii) Uhusiano (Kinyume, maneno husiani) Ulinganishi huu unaonesha kuwa, KSKK iliingiza vipengele vidogo 14 na kuacha 7 wakati KKK iliingiza vipengele vidogo 12 na kuacha 9. Ni KKK tu iliyoingiza taarifa za ngeli za nomino na uelekezi.

Author Biography

E.K.F Chiduo, University of Dar es Salaam
Baraza la Kiswahili la Taifa BAKITA
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X