Main Article Content

Ruwaza za kimofolojia za majina ya mahali ya kihaya: mtazamo wa mofolojia leksika


Adventina Buberwa

Abstract

Makala haya yamechunguza ruwaza za majina ya mahali ya Kihaya1 kwa kuchanganua vijenzi mbalimbali vinavyojenga majina hayo. Data iliyochunguzwa ni sehemu ya data iliyokusanywa kutoka katika wilaya za Muleba, Missenyi, Bukoba Vijijini na Bukoba Mjini, mkoani Kagera kwa ajili ya tasnifu ya Uzamivu. Uchanganuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Mofolojia Leksika kwa mujibu wa Kiparsky (1982) inayosisitiza kuwa vipashio vinavyounda maneno vimepangwa kidarajia kimsonge ambapo vipashio vidogo huungana ili kuunda vipashio vikubwa. Data za utafiti huu zimewasilishwa kwa kutumia majedwali. Hata hivyo, baadhi ya data zimewasilishwa kwa kutumia michoroti ili kudadavua vyema mpangilio wa vipashio vinavyounda majina husika na kuonesha jinsi vipashio hivyo vilivyopangwa kidarajia kimsonge. Matokeo ya uchanganuzi huo yamedhihirisha kuwa majina ya mahali yaliyochunguzwa yameundwa kwa vijenzi mbalimbali ambavyo vimechanganuliwa kimofolojia. Tofauti na madai ya baadhi ya wanaisimu kuwa majina ya mahali yameundwa na mizizi au mashina tu, makala haya yamethibisha kuwa vipo vipashio maalumu vinavyounda majina ya mahali na vinaweza kuchanganuliwa kimofolojia.

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886