Main Article Content

Mikakati ya Uchambuzi wa Fasihi ya Watoto: Mtazamo wa Upokezi wa Msomaji


Pamela M.Y. Ngugi

Abstract

“Fasihi ni kama ndovu, nasi kama wafasili tunaweza kugusa sehemu mbalimbali za mwili wake kujua alivyo ndovu huyu. Kila mara tunapofanya hivyo, tunagundua jambo jipya. Unapomgusa ndovu huyu leo wakati mikono yako imejaa maji au ina unyevunyevu au hata baada ya miaka mingi, unapata kumjua kwa njia tofauti. Fasihi ni kama ndovu huyu, kila mara unapoisoma unagundua jambo jipya.” (Maoni yaliyotolewa na Prof. Ngugi katika mahojiano baina yake na Dkt. Tom Odhiambo na Julias Sigei, Juni, 2, 2015). Kauli hii aliyotoa Prof. Ngugi inadhihirisha ukweli kuwa msomaji wa kazi yoyote ya fasihi ana nafasi kuu katika harakati ya kuipa maana kazi ya kifasihi. Kila mara msomaji anaposoma kazi ya kifasihi huvyaza maana mpya. Maana hizi anazopata kutoka kazi hiyo hutokana na mazingira ya msomaji, ufahamu wake na uzoefu wa kiusomaji pamoja na muktadha wa msomaji. Makala haya yanalenga kubainisha mikakati ya uchambuzi wa fasihi ya watoto kwa kuegemea mkabala wa Upokezi wa Msomaji hasa kwa kuegemea msimamo wa Rosenblatt (1995) wa “Mapatano katika usomaji.” Mtazamo huu unachukulia kwamba msomaji wa kazi fulani ana mchango mkubwa katika harakati za kuipa maana kazi ya kifasihi.

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886