PROMOTING ACCESS TO AFRICAN RESEARCH

Kiswahili

Log in or Register to get access to full text downloads.

Remember me or RegisterDOWNLOAD FULL TEXT Open Access  DOWNLOAD FULL TEXT Subscription or Fee Access

Ufundishaji wa Kiswahili katika Shule za Rwanda: Tathmini ya Makosa, Matatizo na Mahitaji

Cyprien Niyomugabo

Abstract


Utumiaji wa lugha ya pili kwa wanafunzi na walimu waliozoea lugha yao ya kwanza na desturi zao si jambo rahisi. Wakati mwingine, wanatumia lahaja yao ya kijiografia ili waweze kuelewa mambo kadhaa katika lugha ya pili. Je, inawezekana kufundisha lugha ya pili bila uingizaji wa makosa kutoka lugha ya kwanza? Ni mwingiliano upi unaosababisha kufanya makosa katika lugha ya pili? Ni namna gani ya kuyaondoa makosa hayo? Ni lugha gani inayoweza kutumiwa ili kuuondoa mwingiliano huo? Lengo la uchunguzi huu ni kuangalia makosa ya kimwingiliano yanayofanywa na wanafunzi wa Kiswahili kutokana na mahali wanapoishi, pia kutokana na lugha yao ya kwanza ambayo ni Kinyarwanda na kuangalia kategoria ya makosa hayo pia na uhusiano uliopo kati ya mwingiliano na makosa katika lugha ya pili na kuangalia namna ya kurekebisha makosa hayo.AJOL African Journals Online