Main Article Content

Uchanganuzi wa uhamishaji msimbo wa Kiswahili-Kiingereza: mkabala wa Kiunzi cha Lugha Msingi


Shadrack Kirimi Nyagah
Patrick Iribe Mwangi
Basilio Gichobi Mungania

Abstract

Binadamu anapokuwa na ujuzi wa lugha zaidi ya moja huzitumia zote katika mazungumzo yake. Hali hii hujulikana kuwa ni uhamishaji msimbo. Uchanganyaji wa mofimu na elementi za Kiswahili na Kiingereza hufanyika kwa haraka bila kumtatiza mzungumzaji au kukwamiza mawasiliano. Hali hii ndiyo imetupa ari ya kuutafitia uhamishaji huu. Tumeegemea mkabala wa kisarufi kubainisha sifa za kiisimu zinazodhihirika wakati lugha ya Kiswahili na Kiingereza hutumika katika sentensi moja. Makala hii inalenga kudhihirisha ikiwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza hutekeleza majukumu sawa na pili, kutathmini iwapo uhamishaji msimbo hudhibitiwa na sheria za aina yoyote. Tumetumia modeli ya Kiunzi cha Lugha Msingi (K.L.M) ya Myers-Scotton (1993) kusaidia kutimiza malengo hayo. Data ya makala hii imetokana na mazungumzo ya vipindi viwili kutoka kwenye runinga. Uchanganuzi wa data umeonesha kwamba, lugha ya Kiswahili huwa na majukumu mengi ikilinganishwa na lugha ya Kiingereza. Pia, mofimu na elementi za lugha ya Kiingereza huchopekwa kwenye muundo wa Kiswahili kuambatana na sheria za lugha ya Kiswahili.


Journal Identifiers


eISSN: 2591-7013
print ISSN: 2665-0789