Main Article Content

Muundo wa Kirai Kitenzi Katika Lugha ya Kisambaa


N Habibu

Abstract

Utafiti huu umechunguza muundo wa kirai kitenzi katika lugha ya Kisambaa. Mtafiti amebainisha vipashio vinavyoandamana na vitenzi katika sentensi za Kisambaa. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa kitenzi cha Kisambaa kinaweza kisifuatiwe na kipashio chochote au kinaweza kuandamana na vipashio mbalimbali
kama vile kirai nomino, kitenzi kisaidizi, sentensi, kirai kielezi na kirai kihusishi. Hivyo kirai kitenzi cha Kisambaa kinaundwa na kitenzi kimoja; kitenzi na kirai nomino chenye nomino moja au mbili; vitenzi viwili; kitenzi na kiunganishi tegemezi na sentensi; kitenzi, kirai nomino, kiunganishi tegemezi na sentensi; kitenzi na kirai kihusishi; kitenzi na kirai kielezi.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-6739