Main Article Content

Ufafanuzi wa Dhana ya Kiimbo


Boniphace A. Morango

Abstract

Makala haya yanafafanua dhana ya kiimbo ambayo inaonekana kuwa na uvulivuli kuanzia fasili yake. Kiimbo kwa mujibu wa Massamba (2012:159) ni ule mpando-shuko wa sauti wakati wa usemaji, wakati wa uimbaji au wakati wa utoaji ukelele, wa aina yoyote ile. Fasili hii ndiyo inayoonekana kuwa na mashiko zaidi. Ufafanuzi huu wa kiimbo unafanywa kulingana na Nadharia ya Fonolojia Vipandesauti Huru, hiki kikiwa kimojawapo ili vipambasauti vinavyofafanuliwa na nadharia hii. Makala yamebaini fasili mbalimbali za kiimbo, aina, umuhimu, mfanano na tofauti baina ya kiimbo na vitu vingine na mitazamo ya wanaisimu mbalimbali kuhusu dhana ya kiimbo. Makala yamegawanyika katika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza ni utangulizi, ambayo itaelezea usuli wa dhana ya kiimbo. Sehemu ya pili ni kiini, ambayo itafafanua kiimbo ni nini, aina zake, umuhimu na kazi zake na sehemu ya tatu ni hitimisho.

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886