Main Article Content

Makosa Yanayofanywa na Wanafunzi Wanaojifunza Kiswahili kama Lugha ya Pili katika Shule za Sekondari nchini Uganda


Wanyenya Willy

Abstract

Makala haya, yanashughulika na makosa ambayo hufanywa na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya pili katika shule za sekondari nchini Uganda. Mtafiti ameyaainisha makosa mbalimbali na kuyaeleza kiusahihi. Makala yanaeleza namna ambavyo makosa hayo hutokea. Yaani, kama ni makosa yanayosababishwa na mwingiliano wa lugha, ni makosa pitishwa, ni makosa ya usahilishaji au ni makosa ya kimawasiliano. Kwa hiyo makala haya, yamelenga: kutambua makosa yanayofanywa na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya pili na kueleza kiini chayo. Nadhariatete hapa ni kuwa wanafunzi katika shule za sekondari nchini Uganda katika mazungumzo yao na katika maandishi hutumia maneno yanayokaribiana kitahajia na yale ya Kiswahili. Makala yanatokana na utafiti uliofanywa kwa kutumia mbinu ya kushirikisha wanafunzi katika mazungumzo na katika maandishi. Umuhimu wa utafiti huu ni kuwasaidia walimu wanaofundisha Kiswahili katika shule za sekondari kuzingatia na kutatua matatizo ambayo yanabainishwa.

Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886