Main Article Content

Ulinganishi wa mofolojia na sintaksia baina ya lugha 19 za Kibantu za Afrika Mashariki


Hannah Gibson
Gastor Mapunda
Lutz Marten
Julius Taji

Abstract

Katika makala hii tumewasilisha matokeo ya utafiti wetu kuhusu lugha 19 za Kibantu za Afrika Mashariki. Tumeonesha kwamba kuna makundi makuu matatu ambayo yanafanana kiasi cha asilimia 70 au zaidi. Makundi haya yanajikuta katika maeneo mbalimbali ya eneo la utafiti wetu. Kuna kundi la kaskazini, la kati, na la kusini. Tumetumia mbinu maalumu ya kulinganisha mofolojia na sintaksia za lugha hizi, ambayo inatumia vigezo 142 kuelezea kiwango cha ufanano kati yao. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kwamba kuna tofauti kubwa baina ya lugha hizi. Kiwango cha ufanano baina lugha hizi ni kati ya asimilia 45 (yaani uhusiano baina Kikuyu na Kisena) na 80 (baina Kiwabo na Kimakhuwa). Ili kufahamu kwamba kuna makundi maalumu miongoni mwa lugha hizi, tumegawanya lugha ambazo ufanano wao ni chini ya asimilia 70 na zile ambazo ufanano wao ni juu ya asimilia 70. Inawezekana kwamba uhusiano uliopo kati ya makundi haya unaonyesha uhusiano wao wa kihistoria.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886