Main Article Content

Uhusiano wa Taashira na Maisha ya Shujaa wa Kitendi: Mifano kutoka Tendi za <i>Nyakiiru Kibi</i> (1997) na <i>Fumo Liyongo</i> (1999)


Winne Mtega

Abstract

Miongoni mwa sifa za msingi za tendi1 ni matumizi ya taashira. Taashira hizo husaidia kueleza juu ya anguko la shujaa pamoja na maendeleo ya shujaa wa tendi. Kwa upande mwingine, inasisitizwa kuwa msingi wa dhana ya taashira ni ishara au alama ambazo hutumika kuashiria kitu fulani. Aidha, imebainika kuwa utanzu wa utendi hutumia kipengele cha taashira katika kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa. Matumizi haya ya taashira huweza kujidhihirisha kwa namna mbalimbali kama vile kutumia mavazi yenye ishara fulani, mandhari, vifaa, wanyama na hata matendo. Makala hii inadhamiria kuchunguza uhusiano uliopo baina ya taashira na maisha ya shujaa wa kiutendi, hasa katika tendi za Kiswahili. Katika kuonesha uhusiano huo, makala hii imeongozwa na nadharia mbili ambazo ni Nadharia ya Semiotiki na Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji. Mawazo makuu ya nadharia hizo yamesaidia katika kufasili taashira hizo, yaani ishara na alama mbalimbali zilizoambatana na maisha ya  mashujaa hao pamoja na kuonesha uhusiano uliopo baina ya taashira hizo na maisha yake.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886