Main Article Content

Tafsiri kama Nyenzo ya Kutandawaza Utamaduni wa Mswahili: Mfano wa <i>Siku Njema</i> (1996) na <i>A Good Day</i> (2019)


Sarah Ndanu M. Ngesu
George Mrikaria

Abstract

Lengo la makala hii ni kujadili mchango wa tafsiri katika kutandawaza utamaduni wa Mswahili kwa kuangazia riwaya ya A Good Day (Walibora, 2019) kama tafsiri ya riwaya ya Siku Njema (Walibora, 1996) iliyotafsiriwa na Dorothy Kweyu na Fortunatus Kawegere. Tafsiri imekuwa nyenzo muhimu ya kusambaza maarifa ambayo kinadharia yanahusu vipengele vya kiutamaduni kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa. Makala hii inaangazia mwamko wa hivi karibuni wa kutafsiri kazi za fasihi kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Kulingana na Kimutai (2016) na Ngesu na wenzake (2019), kumekuwa na mwamko mpya wa kutafsiri kazi za Kiswahili kwenda Kiingereza na lugha nyinginezo, kinyume na ilivyokuwa awali ambapo kazi mbalimbali zilikuwa zikitafsiriwa kwa wingi kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kusoma na kuchambua matini chanzi na matini lengwa. Makala hii ililenga kuangazia vipengele vya kiutamaduni vilivyohawilishwa kutoka utamaduni chanzi na kuingizwa katika utamaduni lengwa katika matini teule. Modeli ya Newmark (2003) kuhusu ubainishaji wa vipengele vya kiutamaduni iliongoza uchanganuzi wa data za makala hii. Aidha, mbinu linganishi ilitumiwa kuchanganua kiulinganishi matini chanzi na matini lengwa. Mkabala wa kitaamuli ulitumiwa katika uwasilishaji wa data katika majedwali. Matokeo yanaonesha kwamba kupitia njia ya tafsiri, vipengele vya kiutamaduni vimehawilishwa kutoka lugha chanzi kwenda lugha lengwa.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886