Main Article Content

Kukua kwa Matumizi ya Kiswahili Duniani na Utamaduni wake*


Abdulaziz Yusuf Lodhi

Abstract

Makala hii iliwasilishwa tarehe 7 Julai 2023 mjini Copenhagen, Denmaki kuhusu maendeleo ya Kiswahili duniani. Makala inaeleza historia  ya Kiswahili kwa muhtasari kwa kubainisha jamii za Waswahili, yaani wenyeji wa ukanda wa pwani wa Afrika Mashariki. Aidha, makala  imetaja taasisi mbalimbali zilizoanzishwa kwa ajili ya kukuza Kiswahili. Kiswahili kinafundishwa katika taasisi mbalimbali katika maeneo  mbalimbali duniani. Mwandishi amedokeza pia ukrioli wa utamaduni wa Kiswahili kwa kubainisha athari za mila mbalimbali katika  Kiswahili, zikiwamo tasnia za sheria, kilimo, biashara na matibabu. Mwisho, mwandishi amedokeza msamiati wa Kiswahili kutoka katika  lugha mbalimbali za Kiafrika na nje ya bara la Afrika, kutoka Ulaya na Asia.


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886