Main Article Content

Uzoefu wa Ufundishaji na Ujifunzaji wa Kiswahili nchini Ghana


Joshua Agbozo

Abstract

Makaka hii inalenga kufafanua kuhusu uzoefu wa ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili nchini Ghana. Kwa miaka mingi, suala la uzoefu  wa ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili nchini Ghana halijafafanuliwa na wanaisimu ama walimu wa Kiswahili. Makaka hii, kwa  kuongozwa na Nadharia ya Isimujamii (Trudgill, 1983; Hudson, 1985; Mekacha, 2000; Msanjila, Kihore na Massamba, 2011) inajadili uzoefu  wa ufundishaji na ujifunzaji. Aidha, mwandishi alitumia uzoefu wake kwa kuwa alikuwa mwanafunzi wa Kiswahili nchini Ghana  kwa miaka mitano na kufundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni kwa miaka mitatu nchini Ghana na katika nchi za nje aliweza kujadili  uzoefu wa ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili nchini Ghana. Makala hii inajadili historia ya Kiswahili, ufundishaji na ujifunzaji wa  Kiswahili katika taasisi mbalimbali hasa za elimu, changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili nchini Ghana. Pia, makala hii  inatoa mapendekezo kuhusu namna ya kukuza Kiswahili nchini Ghana na duniani kote.  


Journal Identifiers


eISSN: 0023-1886