Main Article Content

Mikabala ya Uchanganuzi wa Viambajengo vya Sentensi na Istilahi Zinazotumika: Mifano kutoka Lugha ya Kiswahili


Fabiola Hassan

Abstract

Uchanganuzi wa viambajengo vya sentensi unaweza kufanywa kwa kutumia mikabala mbalimbali . Kila mkabala unaambatana na matumizi ya  istilahi zake mahususi . Licha ya kuwapo kwa mipaka ya istilahi hizo, bado kuna uchanganyaji wa matumizi yake. Uchanganyaji huu unaashiria  kwamba mikabala ya uchanganuzi wa viambajengo vya sentensi na istilahi zinazohusika ni masuala ambayo hayako wazi sana miongoni mwa  wanaisimu. Hivyo, makala haya yanahusu mikabala ya uchanganuzi wa viambajengo vya sentensi na istilahi zinazohusika kwa kutumia mifano  kutoka lugha ya Kiswahili. Data za makala haya zimepatikana kwa njia ya hojaji, usaili na uchambuzi matini. Ufafanuzi wa data umeongozwa na  misingi ya N adharia ya Sarufi Leksia Amilifu ya Bresnan na Kaplan (ya mwishoni mwa miaka ya 1970). Matokeo yanaonesha kwamba viambajengo  vya sentensi vinaweza kuchanganuliwa kimuundo, kiua milifu, kisemantiki na kipragmatiki. Kwa kuzingatia mikabala hii kuna istilahi za kimuundo,  kiuamilifu, kisemantiki na kipragmatiki. Kwa ujumla makala haya yanahitimisha kwamba istilahi za uchanganuzi wa viambajengo vya sentensi  hazitumiki kiholela bali huamuliwa na m i kabala ya uchanganuzi wa viambajengo.


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129