Main Article Content

Athari za Kimaadili Zitokanazo na Nyimbo za Muziki wa Singeli nchini Tanzania


Aaron A. Mukandabvute
Maria Gores

Abstract

Kumekuwa na madai kwamba nyimbo za muziki wa singeli zimechangia kuporomosha maadili ya jamii wakati madai mengine yanaona nyimbo hizo za muziki zina dhima muhimu ya kuleta ustawi wa kimaadili kama muziki wa kawaida wenye kutekeleza majukumu muhimu katika jamii. Kutokana na kuhitilifiana kwa wanazuoni kuhusu umuhimu wa nyimbo za muziki za singeli, makala haya yanakusudia kuchunguza ni kwa namna gani nyimbo hizo zinavyoathiri maadili ya jamii. Uchunguzi huu ulifanyika kwa kufuata mikakati anuwai ya kiuhakiki. Kwanza, ilibainishwa kuwa zipo nyimbo za muziki wa singeli zenye athari chanya na pia athari hasi. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji lengwa ambapo zililengwa nyimbo za muziki wa singeli zinazobeba athari chanya na hasi katika maadili ya jamii. Uchanganuzi wa data umeongozwa na nadharia mbili: Nadharia ya Uhalisia wa Kiafrika na Nadharia ya Muziki Simulizi. Matokeo yanaonesha kwamba nyimbo za muziki wa singeli zinaakisi uhalisi wa matendo adilifu pamoja na matendo yasiyo adilifu yanayotendeka katika jamii ya Waswahili wa Tanzania. Kutokana na ufumbuzi huo, imependekezwa kuwa wasanii wa nyimbo za muziki wa singeli, wanajamii pamoja na taasisi mbalimbali zinazosimamia maadili katika jamii kwa pamoja waendelee kutumia nyimbo za muziki wa singeli kama chombo cha kudumisha maadili na vilevile kukosoa matendo yasiyokubalika katika jamii siyo tu katika jamii ya Waswahili bali hata duniani kote. Imehitimishwa baada ya upembuzi kwamba nyimbo za muziki wa singeli ni kioo cha uhalisia kama matokeo yanavyodhihirisha. Hivyo, makala haya yanashindwa kukubali au kukataa madai kwamba nyimbo za muziki wa singeli ni chanzo cha mmomonyoko wa maadili.


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129