Main Article Content

Ufundishaji na Ujifunzaji wa Somo la Kiswahili Unaozingatia Stadi ya Tafakuri Tunduizi: Mifano kutoka Shule Teule za Sekondari Wilayani Nyagatare


Laurien Tuyishimire
Wallace Kapele Mlaga

Abstract

Makala haya yanajadili kuhusu ufundishaji na tathmini ya masomo ambayo inazingatia stadi ya tafakuri tunduizi. Makala yanaongozwa  na malengo mahususi mawili: Mosi, ni kujadili namna walimu wa Kiswahili wanavyofundisha na kutathmini masomo yao kwa kuzingatia  stadi ya tafakuri tunduizi. Pili, ni kubainisha changamoto zinazowakabili walimu wa Kiswahili wakati wa kufundisha na kutathmini  masomo yao wakizingatia stadi ya tafakuri tunduizi. Data za makala haya zimekusanywa kwa kutumia njia mbili ambazo ni mahojiano na  uchambuzi matini. Data zilizokusanywa zilichambuliwa kimaelezo kwa kuongozwa na Nadharia ya Ujengaji. Matokeo ya utafiti  yamebainisha kwamba, walimu wa Kiswahili wanashindwa kufundisha na kutathmini kwa ukamilifu masomo wanayofundisha kwa  kuzingatia stadi ya tafakuri tunduizi. Hii ni kutokana na kutumia malengo ya ujifunzaji ya kiwango cha chini katika Taksonomia ya Bloom  na kuuliza maswali ambayo yanamtaka mwanafunzi kukariri kile alichosoma badala ya kukihusisha na hali halisi ya maisha. Aidha Makala  yanabainisha sababu za kuwapo kwa dosari na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na dosari hii. 


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129