Main Article Content

Utabirifu wa Makosa ya Utenganishaji na Uunganishaji wa Maneno katika Kiswahili


Rehema Stephano

Abstract

Uandishi ni mchakato unaohitaji umakini ili kinachoandikwa kieleweke kwa msomaji kwa namna iliyokusudiwa na mwandishi. Ikiwa  kueleweka kutazingatiwa, basi, kutakuwa na mawasiliano madhubuti. Hata hivyo, matini mbalimbali zimekuwa na makosa mengi kiasi  cha kukwamisha mawasiliano baina ya mwandishi na msomaji wake. Lengo la makala haya ni kuchunguza utabirifu wa makosa katika  uandishi kwa kumakinikia makosa ya utenganishaji na uunganishaji wa maneno. Nadharia ya Uchanganuzi Makosa ya Corder (1967) imetumika kuchambua na kujadili data za utafiti kwa sababu inahusika na makosa yanayohusiana na lugha na isimu. Data zimekusanywa  kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa matini na usaili. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba makosa ya kutenganisha  na kuunganisha maneno yanatabirika kwa sababu yana uelekeo mmoja. Makosa ya kuunganisha maneno yamegawanyika katika makundi makubwa manne, yaani maneno yenye urejeshi, maneno yenye kiambishi cha umahali na wakati, maneno yanayotokana na  uradidi, na maneno ambatani. Makosa ya kuunganisha maneno yamegawanyika katika makundi mawili ambayo ni mwambatano wa  vitenzi shirikishi vya “kuwa na” na nomino, na viunganishi tegemezi vinavyoanza na “kwa”. Kwa ujumla, makosa haya yanatokana na  uhamishaji wa kanuni moja katika uandishi wa maneno fulani yenye vipashio, hususani viambishi vinavyofanana. Kufuatia matokeo haya, makala haya yanapendekeza waandishi kuzingatia aina na sifa mahususi za maneno na si kujumuisha kanuni zinazotumika kuandika  baadhi ya maneno. 


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129