Main Article Content

Udondoshaji wa Vipashio katika Vichwa vya Magazeti ya Kiswahili


Ezekiel Emanuel Saidi
Luinasia Elikunda Kombe

Abstract

Uandishi wa magazeti umeonekana kuwa wa kipekee kwani hutumia mitindo mbalimbali ya uandishi ukiwamo udondoshaji wa vipashio.  Tafiti zinaonesha kwamba, udondoshaji wa vipashio katika vichwa vya magazeti hufanyika kwa lengo maalumu. Mathalani, inaweza kuwa  ni kwa lengo la uwekevu, kuleta hamasa na mguso kwa msomaji. Licha ya kudhihirika kwa mtindo huu, tafiti zilizochunguza udondoshaji  katika magazeti ya Kiswahili zinataja kiambishi njeo pekee kama kipashio kinachodondoshwa katika uandishi wa vichwa vya magazeti ya  Kiswahili. Aidha, tafiti tangulizi zinaonesha kuwa vipo vipashio vingine vinavyodondoshwa katika uandishi wa vichwa hivyo ambavyo  vinaweza kuchunguzwa kwa mkabala wa kisintaksia. Hali hiyo imeibua ari ya kutaka kuchunguza udondoshaji wa vipashio hivyo na changamoto zake kwa wasomaji. Data za makala haya zilipatikana maktabani katika magazeti teule ya Kiswahili, yaani Mwananchi,  Nipashe, Habari Leo na Uhuru kwa kutumia mbinu ya usomaji na uchambuzi wa matini. Data zilichambuliwa kwa kuzingatia mkabala wa  kitaamuli wakiongozwa na Nadharia Rasmi ya Chomsky (1965). Matokeo ya utafiti uliozaa makala haya yanaonesha kwamba, vipashio  vinavyodondoshwa katika uandishi wa vichwa vya magazeti ni visabiki vya vitenzi visoukomo, kiima cha sentensi tendwa, kiima cha  sentensi tenda, vihusishi, viunganishi na vitenzi. Udondoshaji huu pamoja na kuonekana kama mtindo, vilevile wakati mwingine  umeonekana kuwa na changamoto ya kuleta utata kwa msomaji. 


Journal Identifiers


eISSN: 2546-2202
print ISSN: 0856-0129