PROMOTING ACCESS TO AFRICAN RESEARCH

Kioo cha Lugha

Log in or Register to get access to full text downloads.

Remember me or RegisterDOWNLOAD FULL TEXT Open Access  DOWNLOAD FULL TEXT Subscription or Fee Access

Uimarishaji wa Ujinsuke katika Fasihi ya Kiswahili: Mifano kutoka katika Hadithi Teule za Kiswahili za Watoto

Ernesta S. Mosha

Abstract


Lengo la makala hii ni kuchunguza namna hadithi za watoto za Kiswahili zinavyoweza kutumika kama njia ya kuimarisha ujinsuke1 katika jamii ili kubadili mtazamo hasi kuhusu watoto wa kike na wanawake katika jamii ya Tanzania. Data za mjadala za makala hii zimepatikana kwa kusoma hadithi za watunzi wawili ambao ni Hua (2007) na Mwakoti (2009). Kwa kuongozwa na Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji katika uchambuzi wa data za makala hii, inabainika kuwa hadithi zinaweza kutumiwa kuwajengea watoto wa kike mtazamo chanya na uwezo wa kufanya mambo mbalimbali ili kuimarisha usawa katika jamii. Hivyo, hadithi ni njia mbadala ya kuhimiza juhudi na ubunifu kwa watoto wa kike ili kuweza kushiriki kikamilifu katika shughuli za kisiasa, kiuchumi na kijamii na kuleta mabadiliko katika mila na desturi zoeleka zinazombagua mtoto wa kike.AJOL African Journals Online