Mitindo ya Lugha Inayomsawiri Mwanamke Kiongozi katika Tamthilia za Pango (2003) na Kigogo (2016)

  • Ogonda S. Sinzore
  • Deborah N. Amukowa
  • Beverlyne A. Ambuyo

Abstract

Tafiti nyingi zilizofanywa kumhusu mhusika mwanamke katika tamthilia za Kiswahili zilimsawiri mwanamke kwa ujumla bila kuangazia uongozi wake. Chache zilizoshughulikia mwanamke kiongozi zimefanya hivi bila kuangazia mitindo ya lugha inayochangia kujenga taswira ya mwanamke kiongozi. Mitindo ya lugha ni muhimu katika kuibua maudhui ya kazi ya fasihi. Makala hii ililenga kuchanganua mitindo ya lugha inayomsawiri mwanamke kiongozi katika tamthilia za Pango (Wamitila, 2003) na Kigogo (Kea, 2016). Zimelengwa tamthilia hizi kwa kuwa zimeandikwa baada ya mwaka 2000 ambapo hadhi ya mwanamke kiongozi imeendelea kuimarika na jamii kuonekana kukubali uongozi wa mwanamke. Tamthilia za Pango na Kigogo ziliteuliwa kupitia mbinu ya usampulishaji dhamirifu kwa  kuwa zina wahusika wanawake ambao ni viongozi. Nadharia ya Udenguzi iliyoasisiwa na Derrida (1966) na kuelezwa na Ntarangwi (2004) iliteuliwa kwa ajili ya utafiti huu. Mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo (maudhui) ilitumiwa kukusanya data. Tamthilia teule zilisomwa na data kunukuliwa. Data ilipangwa kisha ikachanganuliwa kwa njia ya uhakiki wa yaliyomo. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo. Imebainika kupitia makala hii kuwa mitindo mbalimbali ya lugha imechangia kujenga taswira ya mwanamke kiongozi katika tamthilia za Pango na Kigogo. 

Published
2021-05-04
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X