Dhima za Mbolezi za Sasa katika Jamii ya Wakinga Waishio Makete, Tanzania

  • Tumaini Juma Sanga

Abstract

Mbolezi ni kipengele muhimu katika utamaduni wa mazishi miongoni mwa jamii za Afrika. Makala hii inalenga kujadili dhima za mbolezi katika jamii ya Wakinga waishio wilaya ya Makete, mkoani Njombe. Uchambuzi wa data uliongozwa na Nadharia ya Ontolojia ya Kibantu. Makala hii inadhihirisha kuwa tafiti zilizotangulia zilieleza kuwa dhima kuu ya mbolezi ni kuliwaza. Makala hii imebaini kuwa mbolezi katika jamii ya Wakinga zina dhima mbalimbali. Baadhi ya dhima hizo ni kuliwaza wafiwa, kuendeleza imani ya kuwa kuna uhai baada ya kifo, kuendeleza umoja na ushirikiano, kuonya na kukosoa mwenendo wa jamii, kuelimisha, kuelezea matatizo ya jamii na utatuzi wake na  kujipatia kipato kwa watendaji wa mbolezi. Kwa hiyo, makala hii inajadili dhima mbalimbali za mbolezi katika jamii ya Wakingambali na dhima iliyozoeleka ya kuliwaza. Dhima hizo zimepatikana kwa kutumia mbinu mbalimbali katika ukusanyaji wa data, badala ya kuchambua mashairi ya mbolezi pekee.

Published
2021-05-04
Section
Articles

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X