Main Article Content

Ruwaza za ujalizaji wa vitenzi vya Kiswahili sanifu


Deograsia Ramadhan Mtego

Abstract

Makala hii inahusu ruwaza za ujalizaji wa vitenzi katika Kiswahili sanifu. Lengo lake ni kufafanua ruwaza za ujalizaji wa vitenzi kwa kubainisha miundo mbalimbali ya vijalizo vya vitenzi vya Kiswahili sanifu. Data zimekusanywa maktabani kwa njia ya upitiaji wa nyaraka na kuchambuliwa kwa kutumia Nadharia ya Msingi ya Isimu ya Dixon (2010). Makala hii inaonesha kuwa wanasarufi wanatofautiana katika kubainisha aina za miundo ya ruwaza za ujalizaji wa vitenzi katika lugha ya Kiswahili kutokana na maendeleo ya kinadharia. Katika sarufi mapokeo, kitenzi kinajalizwa na kirai nomino chenye uamilifu wa yambwa. Pia, katika Sarufi Mfumo Amilifu kitenzi kinajalizwa na kijalizo ambacho kinaweza kuwa kirai nomino au kirai kivumishi. Vilevile, tofauti na mitazamo iliyotangulia, katika nadharia za kimuundo, kama vile za Sarufi Geuzi inaonesha kuwa kitenzi kinaweza kujalizwa na kirai, kishazi au sentensi. Aidha, mitazamo hiyo inadhihirisha kuwapo kwa namna mbalimbali za ujalizaji wa vitenzi ambazo ndizo ruwaza za ujalizaji wa vitenzi. Katika makala hii, ruwaza za ujalizaji wa vitenzi ni miundo mbalimbali ya vijalizo vya vitenzi kutokana na hulka ya kitenzi husika kinavyoweza kujalizwa. Namna hizo ndizo ruwaza za ujalizaji wa vitenzi ambapo kitenzi kinajalizwa na neno, kirai, kishazi na sentensi. Hivyo basi, vitenzi vya Kiswahili vina namna yake ya kujalizwa ambapo kitenzi kinaweza kujalizwa zaidi ya mara moja kwa namna tofauti kutokana na kitenzi kuukilia namna ya ujalizaji wake.


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X