Main Article Content

Athari za Unyambulishaji katika Uelekezi wa Vitenzi vya Lugha ya Kimasai


Anna Lomayani
Perida Mgecha

Abstract

Makala hii inachunguza namna unyambulishaji unavyoathiri uelekezi wa vitenzi katika lugha ya Kimasai. Malengo mahususi ya makala hii ni kubainisha aina za uelekezi, kueleza uelekezi unavyojitokeza na kuchambua namna unyambulishaji unavyoathiri uelekezi wa vitenzi katika lugha ya Kimasai. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Uhusika iliyoasisiwa na Noam Chomsky (1981). Watoataarifa wamepatikana kwa mbinu za usampulishaji tajiriba na tajwa. Data za makala hii zimekusanywa kwa mbinu za tafsiri na ukalimani na uchambuzi wa data umefanyika kwa kutumia mbinu ya kusimba maudhui. Matokeo ya makala hii yanaonesha kuwa lugha ya Kimasai ina  aina tatu za uelekezi ambazo ni uelekezi wa yambwa moja, wa yambwa mbili na wa yambwa kapa. Aidha, utafiti umebaini kuwa katika  lugha ya Kimasai, yambwa hujitokeza baada ya mtenda ambayo ni tofauti na lugha nyingine, kama vile Kiswahili ambapo yambwa hutokea baada ya kitenzi. Kwa upande wa athari za unyambulishaji katika uelekezi wa vitenzi vya lugha ya Kimasai, husababisha kuongezeka, kuhamishwa au kudondoshwa kwa yambwa. Hata hivyo, tafiti zaidi zinazochunguza vipengele vingine vya kiisimu katika  lugha ya Kimasai zinahitajika. 


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X