Main Article Content

Ukarabati wa Mfuatano wa Irabu kama Sababu ya Muunganiko wa Maneno katika Gᴉrᴉmi


Rehema Stephano

Abstract

Mfuatano wa irabu katika lugha nyingi za Kibantu haupendelewi katika mazungumzo. Huepukwa kwa kutumia ukarabati wa namna mbalimbali. Kwa hiyo, makala hii inahusu ukarabati unaofanyika ili kuepukana na kutumia irabu zinazofuatana katika mpaka wa kisintaksia, yaani baina ya maneno yanayofuatana katika Gᴉrᴉmi (F32). Nadharia ya Fonolojia Zalishi Asilia imetumika kuchambua na  kujadili data za makala hii. Mbinu za kukusanya data zilizotumika katika utafiti huu ni mbili: mbinu ya uhakiki wa kisarufi na ya usaili.  Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba, katika Gᴉrᴉmi, ukarabati wa mfuatano wa irabu baina ya neno na neno hufanywa kwa kutumia  michakato mitatu ya kifonolojia ambayo ni mvutano wa irabu, udondoshaji wa irabu na uyeyushaji wa irabu. Ukarabati huo hufanyika  kurahisisha matamshi na mazungumzo. Kufuatia matokeo haya, makala inapendekeza tafiti zaidi kufanyika ili kubaini jinsi mifanyiko ya  kifonolojia inavyokarabati matamshi ya maneno yanayohusisha mfuatano wa irabu katika lugha zingine, hasa za Kibantu. 


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X