Main Article Content

Dhima za Tungo za Malezi katika Fasihi ya Kiswahili: Mifano kutoka Tenzi Teule


Maryam Y. Mwinyi
Shani Omari Mchepange

Abstract

Malezi ni suala muhimu katika jamii na ni dhamira iliyowashughulisha wanafasihi mbalimbali, ikiwamo utenzi. Makala hii imechunguza dhana ya malezi katika tenzi teule ambazo ni: Utenzi wa Mwanakupona, Howani Mwana Howani, Siraji na Utenzi wa Adili kwa kuzingatia  malengo manne mahususi. Makala imechunguza dhima za tenzi teule kifasihi, kijamii na kwa watunzi wenyewe. Nadharia za Sosholojia  ya Fasihi na Mwingilianomatini zimeongoza uandishi wa makala hii. Data za makala zimekusanywa kwa kusoma matini teule na machapisho mengine yanayohusiana na mada hii. Matokeo yanaonesha kwamba watunzi husika wamefanana na kutofautiana katika kuzungumzia malezi. Kwa watunzi wa kike, dhima zilizojitokeza ni kumcha Mwenyezi Mungu, kujipamba na tabia njema, maisha ya ndoa, utii kwa wazazi, usafi na umaridadi pamoja na umuhimu wa elimu na kazi. Kwa watunzi wa kiume dhima zilizojitokeza ni utiifu na  heshima, mapenzi na ndoa, bidii katika kazi, elimu ya kujitegemea, uvumilivu, uadilifu katika ushahidi, kutunza siri na kutimiza ahadi. Kwa  watunzi wote wa kike na kiume, dhima zilizojitokeza kwa kufanana ni mazingatio ya muktadha wa jamii, nafasi ya baba na mama  katika malezi na ukamilifu katika malezi. 


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X