Main Article Content

Nafasi ya Biashara za Kimataifa katika Kukuza Uzungumzaji wa Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Nchini Rwanda


Emmanuel Niyirora
Wallace K. Mlaga

Abstract

Tafiti zinaonesha kwamba lugha ya Kiswahili nchini Rwanda  haizungumzwi vizuri kama lugha nyingine zinazofundishwa nchini  humo.  Ingawa lugha hii haizungumzwi kwa ufasaha, hasa katika shule  za sekondari, wanafunzi wanaojifunza katika baadhi ya shule za  sekondari wanapata fursa ya kuchangamana na wazungumzaji wa  Kiswahili. Wazungumzaji hao ni pamoja na wazazi, jamaa na marafiki wanaofanya biashara za kimataifa za kuvuka mpaka. Jambo hili  husaidia sana katika uimarishaji wa Kiswahili miongoni mwa  wanafunzi.  Makala hii ililenga kutimiza malengo mahususi mawili.  Lengo la kwanza lilikuwa kujadili dhana ya biashara za kimataifa za  kuvuka  mpaka na dhana ya uzungumzaji wa Kiswahili na lengo la pili  lilikuwa kubainisha mchango wa biashara za kimataifa za kuvuka  mpaka  katika uimarishaji wa uzungumzaji wa Kiswahili kwa  wanafunzi wa shule za sekondari nchini Rwanda. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya  Utamaduni Jamii. Mbinu za uchanganuzi wa matini na  mahojiano zilitumiwa kukusanya data. Usampulishaji lengwa ulitumiwa kupata  sampuli ya utafiti kutoka kwenye shule zilizoteuliwa.  Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa biashara za kimataifa za kuvuka  mpaka zina  mchango mkubwa katika uimarishaji wa uzungumzaji wa  Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini Rwanda.  Isitoshe, utafiti  huu umependekeza kuwa walimu wanapaswa kutumia  fursa ya biashara za kimataifa za kuvuka mpaka katika uimarishaji wa  Kiswahili  miongoni mwa wanafunzi wao. 


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X