Main Article Content

Matumizi ya Nahau katika Ujarabati wa Mikakati ya Kisintaksia ya Usimbaji wa Fokasi katika Sentensi za Kiswahili


Elishafati J. Ndumiwe
Amani Lusekelo

Abstract

Usimbaji wa fokasi katika sentensi za lugha za Kibantu hufanyika kwa kutumia mikakati mbalimbali ya kimofolojia, kisintaksia au  kifonolojia (van der Wal, 2009; Yonenda, 2011; Morimoto, 2014; Ndumiwe,  2023). Aidha, kuna mbinu tofautitofauti zinazotumika  kung’amua  ikiwa mikakati madhukura inasimba fokasi au la. Mojawapo ya mbinu  hizo ni matumizi ya nahau. Van der Wal (2016, 2021)  alichunguza  mbinu hiyo katika ung’amuzi wa usimbaji wa fokasi katika lugha za  Kimakua (P31), Kizulu (S42), Kimatengo (N13), Kirundi  (JD62),  Kichangana (S53), Kiganda (JE15), Kinyakyusa (M31), Kibukusu  (JD31c) na Kitharaka (E54). Hata hivyo, hakuna utafiti uliofanyika  katika lugha ya Kiswahili (G42) kuhusu matumizi ya nahau katika  ujarabati wa mikakati ya usimbaji wa fokasi. Kwa hiyo, lengo la  makala  hii ni kuhakiki mikakati ya kisintakisa ya usimbaji wa fokasi  kwa kutumia nahau za Kiswahili. Data zimekusanywa kwa kutumia  mbinu za  usaili na upitiaji wa nyaraka. Data hizo zimechambuliwa  kitaamuli kwa kuongozwa na Nadharia ya Vibadala vya Kisemantiki  (Rooth,  2016). Utafiti huu umebainisha kuwa nahau za Kiswahili  zikiundiwa sentensi kwa kutumia mikakati ya ukasimishaji, upinduzi  wa  viambajengo na utenguaji kushoto, maana ya nahau inatoweka.  Kwa hiyo, utowekaji wa maana ya nahau huthibitisha kuwa mikakati    husika hutumika kusimba fokasi katika lugha ya Kiswahili.


Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X