Main Article Content

Muundo wa Majina ya Mahali katika Kiswahili: Uchunguzi Kifani wa Majina ya Vituo vya Daladala Jijini Dar es Salaam


A Buberwa

Abstract

Wataalamu mbalimbali (taz. Byarushengo na wenzie, 1977; Katamba, 2003; Watters, 2003; Habwe na Karanja, 2004; Matei, 2008; Kihore na wenzie, 2009 na Mwendamseke, 2011) waliofanya tafiti kuhusu vipengele vya kimofolojia vya nomino za Kibantu wamejikita zaidi katika nomino za kawaida ilhali nomino mahususi hususan zinazotaja mahali zikiachwa bila kushughulikiwa. Kutokushughulikiwa kwa eneo hilo labda ni kutokana na madai kuwa nomino mahususi huundwa na mizizi tu na hivyo haziwezi kuchanganuliwa kimofolojia. Madai haya yamewahi kutolewa na wanaisimu kama Agard (1984) na Habwe na Karanja (2007) kwa kutaja machache. Rugemalira (2005) tofauti na Agard (keshatajwa), na Habwe na Karanja (weshatajwa) anaeleza kuwa nomino mahususi (yakiwemo majina ya mahali) hujidhihirisha katika maumbo yake maalumu. Madai haya yanayopingana ndiyo yamechochea raghba ya kuandika makala haya yanayochunguza muundo wa majina ya mahali katika Kiswahili kwa lengo la kubainisha vijenzi mbalimbali vya majina ya vituo vya daladala jijini Dar es Salaam. Makala haya yanaongozwa na madai kwamba baadhi ya nomino zinazotaja mahali zina maumbo yake maalumu na zinaweza kuchanganuliwa kimofolojia.

Journal Identifiers


eISSN: 0856-552X
print ISSN: 0856-552X