Main Article Content

Ufundishaji wa Fasihi ya Watoto katika Shule za Msingi Nchini Kenya


PMY Ngugi

Abstract

Fasihi ya watoto imeendelea kukua na kupanuka katika tanzu zake mbalimbali katika miaka ya hivi karibuni nchini Kenya. Fasihi hii imepata mwamko mpya tangu ijumuishwe katika muhtasari wa masomo ya lugha shuleni. Makala haya yanatathmini hali ya vitabu vya ziada kwa kuzingatia upatikanaji na ufaafu wake na kupendekeza namna watoto wa shule za msingi wanavyoweza kuelekezwa na kuhimizwa kusoma ili kujenga utamaduni wa usomaji miongoni mwao.